Thursday, 10 March 2016

YANGA YAPAA KUELEKEA RWANDA TAYARI KUIVAA APR

Kikosi cha Yanga tayari kimeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa klabu bingwa Afrika dhidi ya APR utakaopigwa Jumamosi March 12, 2016.
Mabingwa hao watetezi wa taji la VPL wameondoka na ndege ya shirika la Rwanda (Rwanda Air).



CHELSEA YAPIGWA TENA 2-1 NA PSG UEFA

Chelsea wameshatoka kwenye Champions League msimu huu na uhakina msimu ujao pia wameshatoka, lakini Hazard ndio amekua headline kwa upande wa Chelsea zaidi ya kufungwa kwa timu yake.
Kama ulifuatilia mchezo vizuri utakua uliona kipindi cha kwanza kilivyoisha Eden Hazard alibadirishana jezi na Angel di Maria ambapo sio utaratibu wa kawaida. Pia wakati ule kila mchezaji anatakiwa ku-focus kwenye mchezo zaidi ya kitu kingine chochote.
Baada ya kufanya vile baadae mashabiki walimzomea mchezaji huyo ambae kwa muda mrefu analalamikiwa kwak kucheza chini ya kiwango ikisemekana anashinikiza kutaka kuhama club ya Chelsea.
Hiddink alisema,“Mashabiki wa Chelsea walikuana haki na ni sawa walivyomzoea Hazard, wana haki ya kuonyesha kutopendezwa na kitu chochote ambacho wanadhani sio sahihi”. Baadae Roy Keane kwenye kituo cha TV pia alimponda Hazard kwa kitendo hicho hicho.
Roy Kean alisema,“Ninaogopa hata kuzungumzia hili swala, mchezaji akiwa kwenye mechi kubwa akili yake yote inatakiwa kuwa kwenye mchezo na sio kitu kingine. Mimi hata mwisho wa mchezo nisingepoteza muda wa kubadirishana jezi, sasa mtu anafanyaje hivyo muda wa half time”.


Wednesday, 9 March 2016

CHELSEA VITANI LEO UEFA DHIDI YA PSG

Macho yote leo yataelekezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge wakati wa mchezo wa marudiano wa Champions League kati ya Chelsea dhidi ya PSG. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa PSG kushinda kwa mabao 2-1ikiwa nyumbani Ufaransa.
Ni mchezo mgumu sana kwa timu zote mbili, hii ni mara ya tatu ndani ya misimu mitatu Chelsea na PSG kukutana kwenye mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Stamford Bridge kuamua nani atasonga mbele kwa hatua inayofuata.
Msimu uliopita PSG ilishinda kwenye muda wa nyongeza licha ya of Zlatan Ibrahimovic kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Msimu wa 2013-14, Demba Ba alikuwa shujaa wa Chelsea baada ya kufunga bao la kuipeleka Chelsea kwenye hatua ya robo fainali chini ya Mourinho.
Licha ya PSG kuwa katika kiwango bora kwenye ligi ya Ufaransa, haikuwa rahisi kwao kupata ushindi mbele ya Chelsea kwenye mchezo wa kwanza.
Free-kick ya Zlatan Ibrahimovic iliyomgonga Jon Obi Mike na kuzama wavuni lakini Mikel alisawazisha bao hilo kabla ya timu hizo kwenda mapumziko. Edinson Cavani akitokea benchi akaipa ushindi klabu yake ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Kuelekea mchezo huo, klabu hiyo ya Ufaransa inawashambuliaji hatari kwenye klabu yao lakini wanakutana na Chelsea yenye safu ngumu ya ulinzi chini ya Guus Hiddink licha ya kukabiliwa na majeruhi kwa baadhi ya nyota wa nafasi hiyo.
The Blues watakosa huduma ya nahodha wao John Terry wakati Diego Costa yeye anatarajiwa kurudi uwanjani baada ya kukosa mchezo dhidi ya Stoke akiwa anakabiliwa na majeruhi.
Chelsea inatarajiwa kuanza na kikosi kilele ambacho kilianza kwenye mchezo wa kwanza jijini Paris huku makinda Bertrand Traore, Kenedy na Ruben Loftus-Cheek wakiwa machaguo ya ziada kwenye benchi.
Chelsea itatemea sana huduma ya Eden Hazard ambaye kwasasa anaonekana kufanya vizuri. Mbelgiji huyo ameanza kuonesha dalili za kuimarika siku za hivi karibuni.
PSG wametaja kikosi kikali ambacho Serge Aurier ni mchezaji ambaye atakosekana kwenye mchezo huo.
Tarajia kumuona Zlatan Ibrahimovic kuongoza safu ya ushambuliaji wakati Cavani yeye atatokea benchi. Uwepo wa Lucas Moura na Angel Di Maria utamfanya Marco Verratti kuanzia benchi.
Kikosi cha Chelsea kinachotarajiwa kuanza: Thibaut Courtois, Cesar Azpilicueta, Gary Cahill, Branislav Ivanovic, Baba Rahman, Jon Obi Mikel, Cesc Fabregas, Willian, Eden Hazard, Oscar na Diego Costa.
Kikosi cha PSG kinachotarajia kuanza: Kevin Trapp, Marquinhos, David Luiz, Thiago Silva, Maxwell, Blaise Matuidi, Thiago Motta, Marco Verratti, Lucas Moura, Angel Di Maria na Zlatan Ibrahimovic.

ARSENAL YATINGA ROBO FAINAL FA CUP

MABINGWA Watetezi wa Emirates FA CUP Arsenal Jana waliichapa Hull City 4-0 huko KC Stadium katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya 5 na kutinga Robo Fainali.

Timu hizo zilitoka 0-0 huko Emirates na kulazimika kurudiana.

Bao za Arsenal hapo Jana zilifungwa na Olivier Giroud na Theo Walcott, kila mmoja akipiga 2.
Kwenye Robo Fainali Arsenal wapo Nyumbani kucheza na Watford.


UWANJA MPYA WA BARCELONA NI BALAA

Barcelona inasababisha mashabiki kusafiri kutoka nchi mbalimbali kwenda Nou Camp kuangalia mechi za nyumbani za club hiyo. Sasa hivi wamewekeza kiasi cha £465 million ambapo inategemewa kukamilika ndani ya miaka 4.
Pia jina la uwanja huo unategemewa kuuza kwa kampuni ambayo haijatajwa na pesa zitakazolipwa zitakua sehemu ya funding ya ukarabati huo.
Design mpya ya uwanja huo ni kazi ya architects kutoka Japan Nikken Sekkei wakishirikiana na Catalan Studios Pascual. Designer wa uwanja huo wamesema, “Uwanja huu utakua rafiki wa mazingira, utatengeneza vivuli vya kutosha kutokana na angle zote za jua na kuwafanya mashabiki wafurahie mechi wakiwa comfortable. Pia uwanja huu utakua kivutio na icon ya hapa “

RONALDO AZOMEWA NA MASHIBIKI WA REAL

Licha ya kufunga goli ambalo limesaidia kwenye ushindi wa Real Madrid Vs Roma kwenye UCL, mashabiki wa Real Madrid wamemzomea mchezaji wao muhimu Cristiano Ronaldo..
Baada ya kitendo hicho kutokea Sergio Ramos moja kwa moja alikua upande wa Ronaldo na kusema kwamba, “Ningependa kuwaambia mashabiki kufikiria kidogo,ninawaheshimu sana lakini vitu visipoenda vizuri inabidi muda wote wawe upande wa wachezaji wao. Mafanikio kwa club ndio kitu ambacho wachezaji wote tunataka. Ronaldo ni mchezaji wa ki historia kwenye kikosi cha Real Madrid, anaendelea kuonyesha ubora kila mwaka”
Ronaldo anasema kwamba alikua qouted vibaya alivyosema wachezaji wenzake wangekua level kama yake basi wasingepoteza mechi dhidi ya Atletico Madrid. Kauli hiyo ndiyo imesababisha mashabiki kumzoea wakiitafsiri kwamba ni kudharau wenzake lakini yeye anasisitiza kwamba alimaanisha wengi walikua na injury lakini yeye hakuwa nayo.

AZAM FC YAELEKEA AFRIKA KUSINI

Klabu ya Azam FC asubuhi ya leo March 9 imesafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu yaBidvest Wits ya Afrika Kusini, utakaochezwa weekend hii na wiki mbili baadae kurudiana uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.


Wednesday, 2 March 2016

MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU UINGEREZA

VINARA wa Ligi Kuu England Leicester City Jana wakiwa kwao King Power Stadium walitoka Sare 2-2 na West Brom wakati Ugenini Mabingwa Watetezi Chelsea wakiibwaga Norwich City.
WBA walitangulia kuifunga Leicester kwa Bao la Dakika ya 11 la Salomon Rondon na Leicester kujibu kwa Bao 2 za Danny Drinkwater na Andy King katika Dakika za 30 na 46 na kuongoza 2-1 hadi Haftaimu.
Craig Gardner alifunga Bao kwa Frikiki na kuipa WBA Sare ya 2-2 ambayo imewaacha Leicester wakiongoza Ligi Pointi 3 mbele ya Tottenham ambao Leo wanaweza kutwaa uongozi ikiwa wataifunga Ugenini Upton Park West Ham.


Jumatano Machi 2
2245 Arsenal v Swansea                 
2245 Stoke v Newcastle                  
2245 West Ham v Tottenham         
2300 Liverpool v Man City               
2300 Man United v Watford
Jumamosi Machi 5
1545 Tottenham v Arsenal

CHELSEA YAZIDI KUCHANJA MBUGA

Chelsea wameshinda mechi yao ya tatu mfulizo kwenye Premier League na mashabiki wa timu hiyo tayari wameanza kuwa na matumaini huenda timu yao ikamaliza msimu wa ligi ikiwa kwenye top six.
Magoli ya Kenedy na Diego Costa yaliisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Norwich bao la Norwich likifungwa dakika za lala salama na Nathan Redmond.
Chelsea sasa wamepanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Premier League juu ya Liverpoo ambayo kwa sasa bado inapambana kupata matokeo mazuri huku kikosi hicho kinachonolewa na mjerumani Jurgen Klopp kikiwa na mechi mbili mkononi.
Story kubwa kwenye mchezo huo ni kuhusu Kenedy mchezaji wa Chelsea ambaye alifunga goli lake la kwanza kwenye Premier League. Pia ndiyo goli la mapema zadi kufungwa hadi sasa kwenye msimu huu, likiwa limefungwa sekunde ya 39 tu tangu mchezo kuanza.

Tuesday, 1 March 2016

VIDEO - KELECHI NWAKALI MNIGERIA KINDA WA MIAKA 17 ALIYESAJILIWA ARSENAL

LECEISTER CITY YAANZA KUJIPANGA KWAAJILI YA UEFA

Kila kitu kinaenda kwa mipango kwenye nchi za wenzetu ndio maana mambo yanaenda vizuri kabisa. Sasa habari mpya kuhusu Leicester City ni kwamba polisi wa eneo hilo wameanza kujipanga kwa ajili ya UEFA Nights.
Usiku wa UEFA huwa ni muda celebration za mechi za UEFA ambapo mashabiki kutoka nchi mbalimbali hutembelea viwanja tofauti kwa ajili ya kushabikia club zao. Sasa hivi kutokana na njisi Leicester inavyoenda askari wa eneo hilo wameanza kujiandaa na UEFA Night licha ya mechi kadhaa kubakia kwenye msimu huu.
Pc Ali Grimsley alisema, “Ni kitu kipya kwetu hapa Leicester, tunaamini kutakua na mechi usiku wa Jumanne na Jumatano msimu ujao hapa. Kuna uwezekano wa clb kama Real Madrid au Barcelona kuja hapa hivyo basi ni lazima kuwe na changamoto kubwa kwa polisi ndio maana tunajiandaa kwa hilo”.
Leicester haijashuhudiwa kwenye European football kwa muda wa miaka 15 iliyopita. Licha ya kubakisa mechi chache hadi ligi iishe, Leicester wana nafasi kubwa ya kucheza UEFA hadi sasa.

MAKALA - BARAKA AKIMCHAMBUA HAJI MANARA WA SIMBA

Na Baraka Mbolembole
Njia pekee ya kutosikia ‘maneno ya kejeli na najisifu’ ya Mkuu wa kitengo cha habari wa klabu bingwa nchini, Jerry Muro ni kuzima TV yako mara tu umuonapo akijiandaa kusema, unaweza kuzima radio yako kabla hujaanza kumsikia akizungumza, kuachana na usomaji wa habari gazetini ambayo moja kwa moja ikionyesha kuwa mtu aliyekaririwa humo ni Muro.
Jerry anaisemea Yanga lakini wakati mwingine anatumia kipaji chake kuwafurahisha mashabiki wa timu yake. Yanga ndiyo inayompa kiburi cha kusema, Jerry na wala hasemi vibaya licha ya kwamba nyakati fulani amekuwa ‘akiwakwangua’ wapinzani wao wakuu Simba SC kwa maneno ya ‘dhihaka.’
Wakati Simba inapojaribu kufanya vizuri, Hajji Manara ambaye ni mkuu wa kitengo cha habari klabuni hapo amekuwa akitoa tambo zake, lakini bahati mbaya ni kwamba timu yake haina muendelezo mzuri wa matokeo hivyo anakosa cha kusema zaidi.
Kutishia kumpeleka mahakamani Muro kwa sababu alizotoa Manara ni dalili za ‘mtu aliyeshindwa.’ Iko wapi Simba ile iliyotoa suluhu-tasa na Yanga, Oktoba, 2014? Ile ilikuwa ‘timu ya matarajio ya mbele kwa klabu’, viongozi waliahidi kwamba timu ile ingeendelezwa na kutunzwa zaidi.
Kulikuwa na vijana 6 waliotoka timu ya pili ( Simba B) wakati, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na golikipa, Manyika Peter Jr wakiongezeka na kutengeneza ‘kundi la yosso 8’ ambalo lilipiga mpira mkubwa licha ya mechi kumalizik 0-0.
Manara alitamba sana katika vyombo vya habari, na alitoa kejeli zake kwa Yanga iliyokuwa na mastaa wa bei mbaya, lakini mambo yakaenda hovyo katika mechi saba mfululizo za mwanzo wa msimu, kwani timu yake haikuwa imepata ushindi wowote katika ligi. Angesema nini? Angemtambia nani?
Muro amekuwa akiwabeza wazi Simba kutokana na mafanikio yao madogo ndani ya uwanja katika msimu wa nne. Amefikia kuwapachika jina la ‘WA-MCHANGANI’ na kuiita timu yake ya Yanga ‘WA-KIMATAIFA.’
Kama Manara ataenda mahakani kumshtaki Muro kwa mambo yao ya usemaji katika klabu zao, atashindwa tena na Muro kwani tayari timu yake imechapwa mara mbili mfululizo katika VPL pia, Muro amekuwa mwenye maneno mengi zaidi ya kebehi kumshinda Manara, na huko katika sheria haitaongopa, itamuweka huru Muro.
Manara tayari ameshindwa uwanjani, ameshindwa nje ya uwanja na ataenda kushindwa mahakamani kama atafikia uamuzi wa kwenda huko kwa sababu tu ya maneno ya kebehi ya Muro.
Njia ya kumfunga mdogo Muro ni Simba kuimarisha kiwango chao ili wawe na matokeo bora yasiyoshuka haraka lakini kuendelea kuwa nyuma ya Yanga ni wazi Muro ataendelea kutamba, ataisema kwa vijembe Simba ambayo imekaa juu ya Yanga kwa wiki moja tu katika misimu mitatu sasa ya VPL.
Nilimsikia Manara katika moja ya vituo vya radio akitishia kuwachukulia  hatua na kuwapeleka mahakamani wale wote wanao iandika vibaya Simba! Ni dalili ya kushindwa zaidi na wazi mambo yataendelea kuwa magumu upande wake kama timu haitapa matokeo mazuri. Simba SC ni ya nani hasa? Kwanini isichambuliwe? Kwanini isitabiriwe kufanya vibaya?
Simba wanaanza kuweweseka wakati mbaya huu, wakae kimya wasikilize habari na kuzichambua, wamtazame Muro azungumzapo na wajiulize kwa nini anasema sana, wasome makala wanazoona mbaya dhidi yao na wajiulize kwanini wanaandikwa kwa ubaya.
Kutishia kwenda mahakamani bila kujua kosa ulilofanyiwa na mtuhumiwa ni kujipotezea muda. Manara mpeleke Muro mahakamani akapate ushindi mwingine muhimu dhidi yako.

GUUS HIDDINK AMPIGA KIJEMBE LVG WA MAN U

Baada ya mechi ya Arsenal Vs Manchester United kilicho pendwa sana sio matokeo peke yake na Rashford, lakini picha ya LVG akijiangusha mbele ya refa wa nje nayo ilisambaa sana.
Hadi sasa imepitia editing nyingi sana kwenye internet ambapo ikihusishwa kwenye vichekesho mbalimbali. Sasa kocha mholanzi mwenzake Guus Hiddink alivyokua kwenye press na waandishi wa habari aliulizwa kuhusu kitendo kile na alimtania kama hivi.
Guus Hiddink,“LVG unaweza kuona jinsi gani analeta Judo uwanjani. Amejidondosha vizuri sana. Mimi nilikua nacheza Judo na kwa jinsi ninavyoona amejidondosha vizuri na mimi naweza kufanya kama vile.”
Kocha wa Chelsea Guus aliwahi kuanzisha kitengo cha Judo akiwa kocha wa PSV kwao Uholanzi. “Nilianzisha kitengo cha Judo na mimi nikiwa mmoja wa wanafunzi kwa lengo la kuleta stamina kwenye team. Simaanishi kwamba wachezaji walete Judo wakiwa uwanjani lakini kuwa imara uwanjani ni muhimu sana ili waweze kutawala mchezo.”
Kwenye Judo kocha Hiddink alianza kuwa na mkanda mweupe ambao ni kwa ajili ya beginners na baadae akaingia wa brown na kuacha.


Monday, 29 February 2016

VIDEO YA WIMBO MPYA WA HARMONIZE FT DIAMOND - BADO

SIMBA YATINGA ROBO FAINAL FA CUP

Jumapili ya February 28 Kombe la FA Tanzania liliendelea kwa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa 16 bora dhidi ya klabu yaSingida United katika dimba la Taifa Dar Es Salaam.
Simba ambao waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupata majeraha ya kufungwa na Yanga katika mechi zao mbili za Ligi Kuu, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-1, hivyo Simba wametinga hatua ya 8 bora ya Kombe hilo.
Magoli ya Simba yalifungwa na Danny Lyanga dakika ya 3, Hamis Kiiza dakika ya 18 na 66, na Awadh Juma dakika ya 82 na 86, wakati goli pekee la Singida United lilifungwa na Paul Malamla dakika ya 90 ya mchezo.

MAN CITY YATWAA CAPITAL ONE CUP

February 28 michezo mingi ilipigwa Uingereza, lakini ukiachana na michezo ya Ligi KuuUingereza bado burudani kubwa ya soka ilikuwa ni katika mchezo wa fainali ya mechi ya Kombe la Ligi, fainali ambayo ilikuwa inazikutanisha Liverpool dhidi ya Man City.
Mechi hiyo ya Liverpool na Man City ilikuwa ngumu kupata mshindi kirahisi, kwani hadi dakika ya 90 zinamalizika, walikuwa wamefungana goli 1-1 goli la Liverpool lilifungwa naPhilippe Coutinho dakika ya 83, baada ya Man City kupata goli la uongozi  dakika ya 49 kupitia kwa Fernandinho ,  hivyo ikalazimika wapigiane mikwaju ya penati.
Kwa upande wa mikwaju ya penati, bahati iliwaangukia Man City, kwani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 3-1,  Leiva,  Coutinho na Lallana ndio walikosa penati kwa upande wa Liverpool, huku upande wa Man City  Fernandinho ndio alikosa penati.

Saturday, 27 February 2016

LUIS VAN GAAL NA KASHESHE YA KUFUKUZWA MAN U

Hatma ya LOUIS VAN GAAL kuendelea kuifundisha Manchester United angalau mpaka mwishoni mwa msimu inazidi kupata wakati mgumu – LVG atakuwa na siku 11 mwezi ujao ambazo zinaweza kuamua hatma yake ndani ya Old Trafford.

Kuanzia Alhamisi March 10 mpaka Jumapili ya tarehe 20 mwezi March – Man United watakuwa na mechi ngumu 4 ambazo zinaweza kuamua msimu wao umalizike vipi.

 Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya mahasimu zao Liverpool katika mechi ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya michuano ya Europa League.  

Siku 3 baadae mnamo March 13 mashetani wekundu wataikaribisha West Ham katika robo fainali ya FA Cup, baada ya hapo utakuja mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool @OldTrafford mnamo March 17, mchezo ambao utafuatiwa na mchezo dhidi ya City pale Etihad mnamo March 20.
Mechi hizi kwa kiasi kikubwa zitatoa picha kamili ya msimu wa United utaishaje – je mbio za nafasi 4 kwenye EPL zitakuwaje, Wataweza kufika nusu fainali ya FA Cup kwa kuitoa West Ham na hatma yao kwenye michuano ya ulaya ipo mikononi mwa Liverpool.
Miaka miwili iliyopita David Moyes alifukuzwa baada ya Red Devils kuthibitishwa kimahesabu kwamba hawatoweza kushiriki kwenye michuano ya ulaya na LVG anaweza kukutana na kilichomkuta mwenzie ikiwa atashindwa kupata matokeo katika mechi hizo muhimu.
Jose Mourinho anatarajiwa kuchukua mikoba ya boss wake wa zamani mwishoni mwa msimu hata hivyo, ingawa matokeo mazuri kwa LVG yanaweza kuendelea kuifanya bodi ya klabu hiyo kuendelea kugawanyika juu ya kuchukua maamuzi dhidi yake – lakini ikiwa atafeli katika mechi hizo muhimu basi bodi itakuwa haina namna zaidi ya kuchukua maamuzi magumu juu yake.
Ikiwa kocha huyo mdachi akafanikiwa kubadilisha upepo na kubeba vikombe vya FA na Europa – basi anaweza kuendelea msimu ujao na kufanikiwa kumaliza mkataba wake wa miaka 3.


GIANNI INFANTINO NDIE RAISI MPYA WA FIFA

Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.
Katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.
Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa moja.
Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita.
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa”.

Friday, 26 February 2016

SUNDAY OLISEH ABWAGA MANYANGA KUIFUNDISHA NIGERIA

Sunday Oliseh ametangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles.

Oliseh ambaye alianza kuinoa timu hiyo Julai 2015 ametangaza kubwaga manyanga asubuhi ya leo ijumaa kupitia ukurasa wake wa rasmi wa Twitter [@SundayOOliseh] baada ya kuwa katika mvutano wa muda mrefu na chama cha soka cha Nigeria NFF.

Oliseh ameeleza kuwa kukosa kuungwa mkono,kutolipwa mshahara kwa wakati,wachezaji na wasaidizi wake kuburuzwa na kutothaminiwa kwa benchi zima la ufundi ni baadhi tu ya sababu zilizofanya afikie uamuzi huo. 

Kwa kumalizia Oliseh ameshukuru kwa kupata nafasi ya kucheza,kuwa nahodha na mwisho kupata fursa ya kuifundisha Nigeria.




LIVERPOOL HIYOO 16 BORA EUROPA LEAGUE

PENATI ya Dakika ya 5 imewapa Liverpool ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Augsburg ya Germany Uwanjani Anfield katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Kwenye Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Germany Wiki iliyopita Timu hizi zilitoka Sare 0-0.
Penati hiyo ya Liverpool ilifungwa na James Milner na ilitolewa kwa madai kuwa Mchezaji wa Augsburg aliunawa Mpira.
Liverpool watamjua mpinzani wao kwenye Raundi inayofuata baada ya Droo itakayofanyika leo ijumaa Februari 26 huko Nyon, Uswisi.


FIFA KUFANYA UCHAGUZI LEO

Shirikisho la soka duniani Fifa litampta kiongozi mpya leo wajumbe 207 watakapokusanyika mjini Zurich, Uswizi kumchagua mrithi wa Sepp Blatter. Blatter, 79, aliongoza shirikisho hilo tangu 1998. Aling’atuka mwaka jana kutokana na tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo.

Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi. Watano hao ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne. Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda. Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki). Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe. 

Kuna mataifa 209 wanachama wa FIFA lakini Kuwait na Indonesia kwa sasa hawashirikishwi, hivyo wajumbe watakaopiga kura ni 207. Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa.


Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na anayepata kura nyingi kutangazwa mshindi. Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi raundi ya pili. Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.



MARCUS RASHFORD SHUJAA WA MAN U

Marcus Rashford alikuwa shujaa ambaye hakutabiriwa usiku wa Alhamisi dhidi ya FC Midtjylland, akifunga magoli mawili katika mechi yake ya kwanza ya kikosi cha kwanza katika ushindi wa 5-1 ambao uliiwezesha United kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-3 na sasa wanaelekea hatua ya 16 bora ya Europa League.

Magoli hayo yalikuja wakati muhimu – na kuipa United uongozi wa 2-1 na kisha 3-1 na kubadili kabisa hali ya mchezo. Rushford alianza mchezo huo baada ya Anthony Martial kuumia wakati akipasha misuli – kabla ya usiku wa Alhamisi alikuwa hafahamiki, nje ya Manchester.

Rashford alizaliwa jijini Manchester mnamo mwaka 1997 na aliwahi kuitumikia Fletcher Moss Junior club, klabu ambayo iliwatengeneza akina Wes Brown, Danny Welbeck na wengine kama Tyler Blackett na Cameron Borthwick-Jackson. Rashford alijiunga na United na ametokea kwenye akademmi za Man United na kufanikiwa kuwakosha walimu wake.

Mashindano ya UEFA Youth League ndio ambayo aliweza kung’ara sana msimu huu, akifunga mara mbili dhidi ya PSV Eindhoven na dhidi ya Wolfsburg. Kocha wa timu ya vijana Nicky Butt, kiungo wa zamani wa United, alimpa unahodha.

Kulikuwepo na ushawishi wa kujiunga na Manchester City kwa Rashford msimu uliopita lakini akaamua kubaki na kuendelea kujifunza. Goli la kwanza la mshambuliaji huyo lilikuja akitokea benchi katika mechi ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Leicester mwezi December 2015.

Rashford alikiwa katika benchi la kikosi cha kwanza cha United kwenye Premier League katika mechi mbili dhidi ya Watford na Leceister mwishoni mwa November. Zote zilikuwa mechi za ugenini na moja walishinda vs Watford (2-1) na nyingine walitoka sare ya 1-1 na Leceister lakini Rashford hakucheza kabisa.
 Rashford bado ana miaka 18 na anajiunga na listi ya wachezaji chipukizi ambao waliifungia United, Wayne Rooney Federico Macheda, Adnan Januzaj lakini Rashford ameweka rekodi ya kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi (Miaka 18 na siku 117) wa United katika michuano ya ulaya – akiivunja rekodi ya George Best – Rashford pia amefunga magoli katika vikosi vya U18, U19, U21 na sasa kikosi cha kwanza.


Thursday, 25 February 2016

MESSI AMZAWADIA JEZI MTOTO ALIYEVAA JEZI YA MFUKO WA PLASTIKI YENYE JINA LAKE

Mvulana wa taifa la Afghanistan ambaye aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii alipovaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina.
BBC ilimsaidia Messi kumtafuta mtoto huyo ambaye anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Argentina.
Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka 5, anatoka katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

Timu ya usimamizi wa Messi ilithibitisha siku ya Alhamisi kwamba Murtaza alitumiwa jezi ya mshambuliaji huyo wa Argentina iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona ambaye ametuzwa kuwa mchezaji bora mara tano.
''Ninampenda Messi na fulana yangu inasema Messi ananipenda,Murtaza alisema,tayari akimuigiza mshambuliaji huyo anavyosheherekea bao lake.
Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja ilioenea katika mitandao ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.
Madai baadaye yalizuka kwamba mvulana huyo ni wa Kikurdi kutoka Iraq na kwamba nyota huyo wa Barcelona alitaka kumtafuta na kumpa jezi nzuri.



CHELSEA YAPANGA KUONGEZA WACHEZAJI


Kwa mujibu wa gazeti la Sun mmiliki wa Chelsea Mrusi Roman Abramovich atamkabidhi kitita cha £130 millioni kocha mpya ajaye kwa ajili ya kuiimarisha timu hiyo iliyopoteana msimu huu.

Sun linazidi kupasha kuwa Abramovich ametenga kitita hicho akitaka kuongeza sura nne mpya kikosini hapo majira ya kiangazi baada ya kuchoshwa na mwendo mbaya wa timu tangu ilipotwaa ubingwa wa ligi kuu England mwezi Mei mwaka jana.

Sura ambazo tayari zimeanza kutajwa tajwa na huenda zikaletwa na kitita hicho ni Arturo Vidal [Bayern Munich] na John Stones [Everton] kwa ajili ya kuimarisha safu za kiungo na ulinzi. Kitita hicho pia kimeripotiwa kuwa huenda kikaongezeka maradufu na kufikia £210 millioni ikiwa Eden Hazard atauzwa kwenda Real Madrid wakati wa majira yajayo ya kiangazi.



EUROPA LEAGUE KUENDELEA TENA LEO

LEO ni Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI za Marudiano na Timu zote 3 za England zinazocheza Mashindano hayo ziko Viwanja vya Nyumbani kusaka ushindi ili kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Man United wapo kwao Old Trafford huku Wiki iliyopita huko Denmark, wakichapwa 2-1 na FC Midtjylland, na hivyo Leo ni ushindi tu ndio utawakomboa.
Huko Anfield, Liverpool wanatinga kurudiana na Augsburg ya Germany ambayo walitoka nayo 0-0 huko Germany Wiki iliyopita na hivyo ushindi au Sare yeyote ya Magoli ni faida kwao.
Nako huko White Hart Lane Jijini London, Wenyeji Tottenham Hotspur watacheza na Fiorentina ya Italy ambayo walitoka nayo 1-1 na sasa ushindi au Sare ya 0-0 itawafaa Spurs.
Lakini Sare yeyote ya kuanzia 2-2 kwenda juu itawatupa nje Spurs.

Jumatano Februari 24
Sporting Braga 2 Sion 2 [Bao 4-3 kwa Mechi mbili]
Alhamisi Februari 25
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
1800 Lokomotiv Moscow v Fenerbahce [0-2]
1800 Athletic Bilbao v Marseille [1-0]
1800 Bayer Leverkusen v Marseille [1-0]
1800 Rapid Vienna v Valencia [0-6]
1800 Liverpool v Augsburg [0-0]
1800 Krasnodar v Sparta Prague [0-1]
1800 Lazio v Galatasaray [1-1]
1800 Schalke v Shakhtar Donetsk [0-0]
2305 Molde v Sevilla [0-3]
2305 Napoli v Villarreal [0-1]
2305 Porto v Borussia Dortmund [0-2]
2305 Olympiacos v Anderlecht [0-1]
2305 Tottenham v Fiorentina [1-1]
2305 Basle v St Etienne [2-3]
2305 Manchester United v FC Midtjylland [1-2]