Sunday Oliseh ametangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu
ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles.
Oliseh ambaye alianza kuinoa timu hiyo Julai 2015 ametangaza
kubwaga manyanga asubuhi ya leo ijumaa kupitia ukurasa wake wa rasmi wa Twitter
[@SundayOOliseh] baada ya kuwa katika mvutano wa muda mrefu na chama cha soka
cha Nigeria NFF.
Oliseh ameeleza kuwa kukosa kuungwa mkono,kutolipwa
mshahara kwa wakati,wachezaji na wasaidizi wake kuburuzwa na kutothaminiwa kwa
benchi zima la ufundi ni baadhi tu ya sababu zilizofanya afikie uamuzi huo.
Kwa
kumalizia Oliseh ameshukuru kwa kupata nafasi ya kucheza,kuwa nahodha na mwisho
kupata fursa ya kuifundisha Nigeria.

No comments:
Post a Comment