City ambayo ilikuwa ugenini kucheza dhidi ya Dynamo Kyiv, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.
Magoli ya City yalifungwa kuanzia dakika ya 15 kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero, dakika ya 40 David Silva akapachika goli la pili, kipindi cha pili Dynamo Kyiv walirudi na kusawazisha goli moja kupitia Vitaly Buyalsky dakika ya 58, Yaya Toure akashindilia msumari wa mwisho dakika ya 90.
Kwa upande mwingine Atletico Madrid walitoka sare ya 0-0 na PSV.

No comments:
Post a Comment