Thursday, 10 March 2016

YANGA YAPAA KUELEKEA RWANDA TAYARI KUIVAA APR

Kikosi cha Yanga tayari kimeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa klabu bingwa Afrika dhidi ya APR utakaopigwa Jumamosi March 12, 2016.
Mabingwa hao watetezi wa taji la VPL wameondoka na ndege ya shirika la Rwanda (Rwanda Air).



CHELSEA YAPIGWA TENA 2-1 NA PSG UEFA

Chelsea wameshatoka kwenye Champions League msimu huu na uhakina msimu ujao pia wameshatoka, lakini Hazard ndio amekua headline kwa upande wa Chelsea zaidi ya kufungwa kwa timu yake.
Kama ulifuatilia mchezo vizuri utakua uliona kipindi cha kwanza kilivyoisha Eden Hazard alibadirishana jezi na Angel di Maria ambapo sio utaratibu wa kawaida. Pia wakati ule kila mchezaji anatakiwa ku-focus kwenye mchezo zaidi ya kitu kingine chochote.
Baada ya kufanya vile baadae mashabiki walimzomea mchezaji huyo ambae kwa muda mrefu analalamikiwa kwak kucheza chini ya kiwango ikisemekana anashinikiza kutaka kuhama club ya Chelsea.
Hiddink alisema,“Mashabiki wa Chelsea walikuana haki na ni sawa walivyomzoea Hazard, wana haki ya kuonyesha kutopendezwa na kitu chochote ambacho wanadhani sio sahihi”. Baadae Roy Keane kwenye kituo cha TV pia alimponda Hazard kwa kitendo hicho hicho.
Roy Kean alisema,“Ninaogopa hata kuzungumzia hili swala, mchezaji akiwa kwenye mechi kubwa akili yake yote inatakiwa kuwa kwenye mchezo na sio kitu kingine. Mimi hata mwisho wa mchezo nisingepoteza muda wa kubadirishana jezi, sasa mtu anafanyaje hivyo muda wa half time”.


Wednesday, 9 March 2016

CHELSEA VITANI LEO UEFA DHIDI YA PSG

Macho yote leo yataelekezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge wakati wa mchezo wa marudiano wa Champions League kati ya Chelsea dhidi ya PSG. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa PSG kushinda kwa mabao 2-1ikiwa nyumbani Ufaransa.
Ni mchezo mgumu sana kwa timu zote mbili, hii ni mara ya tatu ndani ya misimu mitatu Chelsea na PSG kukutana kwenye mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Stamford Bridge kuamua nani atasonga mbele kwa hatua inayofuata.
Msimu uliopita PSG ilishinda kwenye muda wa nyongeza licha ya of Zlatan Ibrahimovic kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Msimu wa 2013-14, Demba Ba alikuwa shujaa wa Chelsea baada ya kufunga bao la kuipeleka Chelsea kwenye hatua ya robo fainali chini ya Mourinho.
Licha ya PSG kuwa katika kiwango bora kwenye ligi ya Ufaransa, haikuwa rahisi kwao kupata ushindi mbele ya Chelsea kwenye mchezo wa kwanza.
Free-kick ya Zlatan Ibrahimovic iliyomgonga Jon Obi Mike na kuzama wavuni lakini Mikel alisawazisha bao hilo kabla ya timu hizo kwenda mapumziko. Edinson Cavani akitokea benchi akaipa ushindi klabu yake ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Kuelekea mchezo huo, klabu hiyo ya Ufaransa inawashambuliaji hatari kwenye klabu yao lakini wanakutana na Chelsea yenye safu ngumu ya ulinzi chini ya Guus Hiddink licha ya kukabiliwa na majeruhi kwa baadhi ya nyota wa nafasi hiyo.
The Blues watakosa huduma ya nahodha wao John Terry wakati Diego Costa yeye anatarajiwa kurudi uwanjani baada ya kukosa mchezo dhidi ya Stoke akiwa anakabiliwa na majeruhi.
Chelsea inatarajiwa kuanza na kikosi kilele ambacho kilianza kwenye mchezo wa kwanza jijini Paris huku makinda Bertrand Traore, Kenedy na Ruben Loftus-Cheek wakiwa machaguo ya ziada kwenye benchi.
Chelsea itatemea sana huduma ya Eden Hazard ambaye kwasasa anaonekana kufanya vizuri. Mbelgiji huyo ameanza kuonesha dalili za kuimarika siku za hivi karibuni.
PSG wametaja kikosi kikali ambacho Serge Aurier ni mchezaji ambaye atakosekana kwenye mchezo huo.
Tarajia kumuona Zlatan Ibrahimovic kuongoza safu ya ushambuliaji wakati Cavani yeye atatokea benchi. Uwepo wa Lucas Moura na Angel Di Maria utamfanya Marco Verratti kuanzia benchi.
Kikosi cha Chelsea kinachotarajiwa kuanza: Thibaut Courtois, Cesar Azpilicueta, Gary Cahill, Branislav Ivanovic, Baba Rahman, Jon Obi Mikel, Cesc Fabregas, Willian, Eden Hazard, Oscar na Diego Costa.
Kikosi cha PSG kinachotarajia kuanza: Kevin Trapp, Marquinhos, David Luiz, Thiago Silva, Maxwell, Blaise Matuidi, Thiago Motta, Marco Verratti, Lucas Moura, Angel Di Maria na Zlatan Ibrahimovic.

ARSENAL YATINGA ROBO FAINAL FA CUP

MABINGWA Watetezi wa Emirates FA CUP Arsenal Jana waliichapa Hull City 4-0 huko KC Stadium katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya 5 na kutinga Robo Fainali.

Timu hizo zilitoka 0-0 huko Emirates na kulazimika kurudiana.

Bao za Arsenal hapo Jana zilifungwa na Olivier Giroud na Theo Walcott, kila mmoja akipiga 2.
Kwenye Robo Fainali Arsenal wapo Nyumbani kucheza na Watford.


UWANJA MPYA WA BARCELONA NI BALAA

Barcelona inasababisha mashabiki kusafiri kutoka nchi mbalimbali kwenda Nou Camp kuangalia mechi za nyumbani za club hiyo. Sasa hivi wamewekeza kiasi cha £465 million ambapo inategemewa kukamilika ndani ya miaka 4.
Pia jina la uwanja huo unategemewa kuuza kwa kampuni ambayo haijatajwa na pesa zitakazolipwa zitakua sehemu ya funding ya ukarabati huo.
Design mpya ya uwanja huo ni kazi ya architects kutoka Japan Nikken Sekkei wakishirikiana na Catalan Studios Pascual. Designer wa uwanja huo wamesema, “Uwanja huu utakua rafiki wa mazingira, utatengeneza vivuli vya kutosha kutokana na angle zote za jua na kuwafanya mashabiki wafurahie mechi wakiwa comfortable. Pia uwanja huu utakua kivutio na icon ya hapa “

RONALDO AZOMEWA NA MASHIBIKI WA REAL

Licha ya kufunga goli ambalo limesaidia kwenye ushindi wa Real Madrid Vs Roma kwenye UCL, mashabiki wa Real Madrid wamemzomea mchezaji wao muhimu Cristiano Ronaldo..
Baada ya kitendo hicho kutokea Sergio Ramos moja kwa moja alikua upande wa Ronaldo na kusema kwamba, “Ningependa kuwaambia mashabiki kufikiria kidogo,ninawaheshimu sana lakini vitu visipoenda vizuri inabidi muda wote wawe upande wa wachezaji wao. Mafanikio kwa club ndio kitu ambacho wachezaji wote tunataka. Ronaldo ni mchezaji wa ki historia kwenye kikosi cha Real Madrid, anaendelea kuonyesha ubora kila mwaka”
Ronaldo anasema kwamba alikua qouted vibaya alivyosema wachezaji wenzake wangekua level kama yake basi wasingepoteza mechi dhidi ya Atletico Madrid. Kauli hiyo ndiyo imesababisha mashabiki kumzoea wakiitafsiri kwamba ni kudharau wenzake lakini yeye anasisitiza kwamba alimaanisha wengi walikua na injury lakini yeye hakuwa nayo.

AZAM FC YAELEKEA AFRIKA KUSINI

Klabu ya Azam FC asubuhi ya leo March 9 imesafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu yaBidvest Wits ya Afrika Kusini, utakaochezwa weekend hii na wiki mbili baadae kurudiana uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.